About Juhudi Saccos Ltd
Juhudi Saccos Ltd is an accounting, located at Box 42825, 255 Dar es Salaam, Tanzania. Visit their website juhudisaccos.blogspot.com for more detailed information.
Juhudi Cooperative and Credit Society (Juhudi Saccos Ltd) ni ushirika wa akiba na mikopo unaoundwa na wakazi wa Mzinga - Kibeberu mkoani Dar es Salaam.
Tags
Juhudi Cooperative and Credit Society (Juhudi Saccos Ltd) ni ushirika wa akiba na mikopo unaoundwa na wakazi wa Mzinga - Kibeberu mkoani Dar es Salaam, ushirika huu umesajiliwa mnamo tarehe 20 ya mwezi wa kwanza mwaka 2014 (20/01/2014) kama asasi ya kutoa huduma za kifedha chini ya sheria ya vyama vya ushirika namba 20 ya mwaka 2003.
Dira
Kuwa taasisi bora ya ushirika wa akiba na mikopo yenye riba na masharti nafuu na inayoongoza kwenye utoaji wa huduma za kifedha ndani na nje ya nchi ya Tanzania
Dhima
Kukusanya akiba na amana kwa ajili ya kuwakopesha wanachama kwa riba na masharti nafuu na kuwaelimisha namna ya kutumia mikopo hiyo kwa busara ili kuwajengea uwezo mkubwa wa kiuchumi na maisha bora
Madhumuni
Kusaidiana, kustawisha na kuwezeshana katika shughuli za ujenzi wa taifa kwa kufuata taratibu na misingi ya ushirika na vilevile kudumisha upendo na ushirikiano kati yetu.
Ili kuweza kuyafikia mambo hayo yote, ushirika huu utafanya yafuatayo:-
Kupokea hisa, akiba na amana toka kwa wanachama
Kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa wanachama
Kuwashawishi watu ambao si wanachama kujiunga na ushirika huu
Kukuza akiba za wanachama kwa kuwahimiza kuongeza hisa, akiba na amana zao mara kwa mara
Kuhifadhi katika mashirika ya fedha na kununua dhamana za serikali baada ya kutoa huduma ya Akiba na Mikopo kwa wanachama
Kuanzisha na kuendeleza shughuli zozote za kiuchumi kwa manufaa ya wanachama kama itakavyokubaliwa katika mkutano mkuu
Kupambana na umaskini, ujinga , maradhi na ubaguzi hasa wa kijinsia
Kujenga chama chenye uwezo wa kujiendesha chenyewe na kukidhi mahitaji ya huduma za kifedha kwa wanachama wake na kuchochea msukumo wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kuwa sehemu ya mtandao wa huduma za kifedha katika misingi na taratibu za ushirikiano