Vynest Logo
Search
Add Listing

About Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni

Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni is a company, located at Arusha, Arusha Region, Tanzania. Visit their website www.wamisionariwakatoliki.or.tz or LinkedIn profile for more detailed information.

Kundi la Wamisionari Wakatoliki Mtandaoni lilianzishwa mwaka 2010 wakati huo likiitwa Vijana Wakatoliki Tanzania, baada ya viongozi wa Vijana wa Parokia ya Familia Takatifu Njiro Jimbo kuu la Arusha kupata wazo la kuunganisha vijana wote Wakatoliki wa Tanzania kupitia Mtandao wa Facebook. Kundi hilo hapo awali lilipewa jina la VIWAWA FAMILIA TAKATIFU –NJIRO. Kundi lilipata umaarufu na kujulikana zaidi baada ya kongamano la Vijana Kitaifa lililofanyika Jimbo Kuu la Arusha 5-9 September 2011 na hivyo ikalazimika kubadili jina na kuliita VIJANA WAKATOLIKI TANZANIA ili kukidhi mahitaji ya wanachama walioanza kujiunga baada ya kongamano maana walitoka kila kona ya Tanzania.Kijana yeyote Mkatoliki anapokelewa kujiunga na kundi. Tuna kila aina ya vijana na wasio vijana kwenye kundi wakiwemo Viongozi na wanachama wa Viwawa kutoka majimbo mengi ya Tanzania, Vijana ambao hawafungamani na chama chochote (Vijana Walei), Mashemasi, Mapadre na walei wengine. Hadi sasa Kikundi kina wanachama wapatao kwenye Mtandao wa Facebook Zaidi ya 9000 na wanachama 80 ambao ndio walio hai na wanaoshiriki shughuli za mara kwa mara za utume kwenye mitandao. Kwa sasa tunapatikana katika mitandao ya whatsap, instagram, telegram na kwa sasa tupo kwenye hatua ya mwisho ya kuanzisha website yetu.Kati ya mambo ya msingi yanayofanywa ndani ya kundi ni Elimu juu ya Imani Katoliki. Kundi limekuwa msaada mkubwa kwa vijana wanaohitaji kuelimishwa juu ya jambo lolote ama changamoto yoyote kwenye imani Katoliki. Mashemasi na Mapadre walioko kwenye kundi wamekuwa msaada mkubwa kwa kujibu maswali mengi kwa ufasaha. Tunaamini tumetoa mchango mkubwa katika kuwasaidia Vijana kuielewa imani yao.Aidha tunajivunia kuwa kati ya wadau waliokuwa mstari wa mbele kuhakikisha filamu iitwayo SISTER MARY, ambayo kwa macho yetu ilikuwa ikidhalilisha Ukatoliki iliyotarajiwa kusambazwa mwaka 2014 haitoki. Harakati zetu ziliwezesha filamu hiyo kuzuiwa kusambazwa.Read more...... https://wamisionariwakatoliki.or.tz/

Tags

Map

Add Reviews & Rate item

Your rating for this listing :